Ijumaa 18 Julai 2025 - 08:43
Wakati mtoto anapouliza swali, ni vipi yatupasa kumjibu? + Njia saba za kimatendo

Hawza/ Watoto, kwa shauku yao ya kujua na uwezo wa kufikiria, hutaka kuielewa dunia inayowazunguka. Wazazi kwa subira, heshima, na kutumia mbinu rahisi na zinazofahamika wanaweza kujibu maswali yao kwa njia bora kabisa.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, shauku ya kujua watoto ni dirisha linalofunguka kuelekea ulimwengu wa maajabu, wazazi kwa majibu ya kielimu na lugha laini ya kupendeza, huwa ni wasanifu wa fikra za watoto wao.

Utangulizi

Akili ya mtoto ni kama bustani changa inayomea kwa kila swali linaloulizwa yanachipusha matawi mapya. Kwa hamu yao isiyo na mwisho ya kujua na fikra zao zenye uhai, wanatafuta maana na sababu ya kila jambo wanaloliona au wasiloliona ulimwenguni.

Maswali yao yanayoonekana kuwa mepesi, mara nyingi yana mizizi katika fikra za kina na juhudi ya kuelewa maana za mambo magumu, wazazi, kwa kutunza utulivu, ukweli na heshima kwa akili ya mtoto, wanaweza kuwa wafuasi wao bora katika njia ya kuyajibu maswali hayo.

Mbinu za kushughulikia maswali ya watoto

1. Kabla ya kujibu, kuwa msikilizaji wa kweli

Wakati mwingine watoto hawaulizi swali kwa ajili ya kupata jibu tu, bali wanatafuta usalama na kueleweka. Mtoto wako anapouliza: “Kama Mungu ni mwenye huruma, kwa nini kuna vita?”
Badala ya kuharakisha jibu, mwambie: “Swali zuri sana umeniuliza; wewe mwenyewe unafikiriaje?” Kisha, msikilize kwa makini ili uelewe kinachomsumbua.

2. Tumia mifano ya maisha ya kila siku ya mtoto

Kama mtoto wako hupenda michezo ya video au simu, mwambie:
“Umeona ile hali mchezo unapokwama, mtaalamu wa programu lazima auisahihishe? Hali ya ulimwengu pia ina mpangaji, kama mchezo una lengo, maisha pia yana lengo.”

3. Epuka kauli za kejeli au za dharau

Kauli kama vile “Wewe unaelewa nini kuhusu dini?” au “Mtoto hapaswi kuuliza maswali kama haya,” huzaa kuficha mambo na ukaidi wa makusudi.

4. Kama hujui, andamana naye usikwepe

Mtoto akikuuliza, “Kwa nini baadhi ya watu wasio na dini wanafanikiwa zaidi?” na huna jibu, mwambie tu kwa urahisi:
“Swali zuri sana, hebu tutafute jibu lake pamoja.”
Kwa kufanya hivi, unamfundisha kuwa kuuliza maswali si kosa.

5. Tumia vyanzo sahihi na rahisi

Watoto hupendelea maelezo mafupi yenye picha au vielelezo, ikiwa hoja ni ngumu, mpelekee video fupi ya dakika mbili, si hotuba ya saa moja!

6. Fanya mazingira ya mazungumzo nyumbani kuwa salama

Mtoto wako akihisi kuwa kila swali litamletea maonyo, ataacha kuuliza kabisa, badala yake, atatafuta majibu mahali pengine na huenda mahali pasipo sahihi kwa malezi yake.

7.Tumia lugha rahisi

Watoto huhitaji majibu yaeleweke kirahisi, epuka istilahi ngumu au za kielimu, jitahidi kueleza mambo kwa lugha ya moja kwa moja na inayolingana na uwezo wao wa kuelewa.

Mbinu Muhimu na ya Kimkakati

Wazazi wanapaswa kuwa na subira mbele ya maswali ya watoto wao na kuwashughulikia kwa kutumia mbinu zifuatazo:

Uliza anachokijua mtoto: Mwombe mtoto aeleze yote anayoyajua kuhusu mada hiyo.

Chochea fikra za mtoto: Muulize, “Wewe unafikiriaje?” au “Kwa mtazamo wako, hali itakuwaje?”

Mfanye afikirie hali tofauti: Kwa kuuliza maswali kama, “Unaonaje ikiwa itakuwa hivi?” msaidie kufikiria pande tofauti za swali lake.

Mfano wa swali la kawaida la mtoto:

“Mama, kwa nini anga inakuwa giza?”
Usimpe jibu moja kwa moja, badala yake, muulize:

“Wakati anga inapokuwa giza, ni mambo gani yanatokea?”
“Ni vitu gani vinavyoonekana angani?”
“Nyota na mwezi huwa tunaweza kuviona lini angani?”

Kwa kuuliza maswali haya, unahusisha zaidi akili ya mtoto katika malezi, kadiri akili ya mtoto inavyoshughulika zaidi, ndivyo mafanikio yanavyoongezeka, kujibu haraka haraka maswali ya mtoto, hakumfai, mtoto anatakiwa achunguze mwenyewe na kufikia uelewa wake, mbinu hizi humsaidia mtoto kufikiri, kuchambua, na kukuza uwezo wa kutatua matatizo.

Mifano ya Maswali na Majibu:

1. Mungu yuko wapi? Kwa nini simuoni!?

Jibu: “Je, unaweza kuona hewa unayoivuta? Hapana! Lakini unajua ipo kwa sababu unaishi. Vivyo hivyo, Mungu yupo kila wakati, hata kama haonekani, kama vile mwanga mkali ulio nyuma ya pazia.”

2. Mungu ana umbo gani?

Jibu: “Yeye ni kama huruma au furaha unaweza kuihisi, lakini huwezi kuiona kwa macho, kama Mungu angekuwa kama binadamu, asingeliweza kuwa kila mahali!”

3. Mama, kwa nini tunaota ndoto? Je, ndoto ni za kweli?

Jibu: “Ndoto ni kama filamu ambazo akili zetu hutengeneza wakati wa usiku, wakati mwingine zinachekesha, wakati mwingine za kushangaza, si za kweli, lakini huwa na baadhi ya mambo kutoka ndani ya hisia zetu.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha